Waone wale: mpenzi, na mwenza wake njiani,
Miili sako kwa bako, mawazo hapa na pale,
Ila swali la kuenzi, shaka haipenyi ndani.
Ama yule ba’skelini, nywele zimepeperushwa,
Basi ubavu kushoto, ya wanaotoka kazi,
Nyuma kwa wingi majani, yavurugwa kwa hewa.
Kwenye bustani wachanga, mikoba yao ya shule,
Vitini wapumzikao, wengine na mbwa zao,
Nasi tunatangatanga, mioyo pamoja milele.